Thursday, 12 June 2014

Kumekucha Brazil, Dimba kung'oa nanga








Michuano kuanza Brazil

Kombe la dunia Brazil 2014 linatarajiwa kungo'a nanga baadaye leo jioni huku Brazil na Croatia wakitoana kijasho mjini Sao Paolo.

Dimba hilo litakalodumu kwa mwezi mmoja, litashuhudia mataifa 32 yakimenyana kuwania kombe hilo katika fainali itakayochezwa mjini Rio tarehe 13 Julai.





Mechi ya ufunguzi itaanza baada ya sherehe ya kufungua mechi hiyo mjini Sao Paulo. Ni mechi ambayo itakuwa inatoa kipaombele kuonyesha umuhimu wa kukuza vipaji, utu na kabumbu.

"wacheni niwambie kuwa wakati umewadia. Tunaenda sote . Hili ni kombe letu la dunia, '' alinukuliwa akisema kocha wa Brazil Luis Felipe Scolari.

Mwaka jana zaidi ya watu milioni moja walishiriki katika maandamano ya kupinga hatua ya serikali kuandaa michezo hiyo kwa gharama ya juu wakati wananchi wengi wakiishi kwa umasikini.

Serikali ya Brazil iko makini kuzuia kutokea tena kwa ghasia zilizoshuhudiwa wakati wa maandamano hayo. Rais Dilma Rousseff amesema kuwa hatakubali kamwe maandamano yanayosababisha ghasia kuathiri kombe la dunia.

Maelfu ya polisi na wanajeshi watashika doria nchini humo kuhakikisha kuwa mechi zinafanyika bila vurufu.

England itacheza mechi yao ya ufunguzi dhidi ya Italy Jumamosi tarehe 14 , mechi ambayo itapeperushwa moja kwa moja na BBC.

Timu hiyo pia itacheza dhidi ya Uruguay na Costa Rica katika kundi D.

Wenyeji Brazil wataanza mechi leo wakipigiwa upatu kushinda kombe la dunia kwa mara ya sita wakati mabingwa watetezi Hispania nao wanakilenga kushinda kombe hilo kwa mara ya nne baada ya kushinda ubingwa wa Ulaya miaka miwili iliyopita.

Monday, 9 June 2014

Uwanja wa ndege washambuliwa Pakistani



Wanajeshi wa Pakistan wakiwa kwenye uwanja wa ndege wa Karachi kukabiliana na washambulizi.
Mapambano ya risasi yaliyodumu saa tano katika uwanja wa mji mkubwa zaidi nchini Pakistani ,Karachi yamewauwa watu 23 wakiwemo washambuliaji wote 10.
Washambuliaji hao waliokuwa na silaha nzito nzito waliingia sehemu ya majengo ya uwanja huo kupitia njia zinazotumiwa na ndege za mizigo au zile zinazotumiwa kuwapokea wageni wenye hadhi na sifa yaani V.I.Ps.
Walipenya usiku wa manane na kuanza kuwashambulia maafisa usalama kwa gruneti na kwa kuwafyatulia risasi.
Makamanda katika jeshi waliitwa kukabiliana na washambuliaji hao na milio ya risasi ilisikika hadi alfajiri wakati hali ilipodhibitiwa.
Haijabainika vyema ni akina nani hasa walioshambulia lakini yamewahi kufanyika mashambulio kama hayo hasa katika maeneo ya wanajeshi wa angani na wa majini ambapo wanamgambo wa Taliban walihusika

Papa awapokea Peres na Abbas



Mahmoud Abbas, Papa na Shimon Peres Vatikani
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis amewakaribisha Rais wa Israil, Shimon Peres, na mwenzake kutoka Palestina, Mahmoud Abbas, katika maombi ya aina ya kipekee katika makao makuu ya Kanisa Katoliki ya Vatican. Viongozi hao wawili walikutana na Papa nje ya makaazi yake kabla ya kuandamana naye, wakiandamana na kiongozi wa Kanisa la Ordhodoz, Partriarch Artholomew kwa hafula maalumu katika Medani ya Vatican. Akiongea katika hafula hiyo Papa alisema ujasiri na nguvu vinahitjika katika juhudi za kuleta amani.
"Kuleta amani kunahitji ujasiri mkubwa kuliko vita. Kunahitaji ujasiri wa kusema ndio kwa mkutano na La kwa vita; ndio kwa mashauriano na La kwa makabiliano; ndio kwa kuheshimu mikataba na La kwa uchokozi; Ndio kwa ukweli na La kwa Uongo; kwa haya yote tunahitaji ujasiri na nguvu moyoni," Papa alisema
Na katika hotuba yake Bwana Peres alisema alitakia vizazi vyote vijavyo amani ya kudumu:

"Rafiki wapenzi, Nilikuwa mchanga, na sasa nimezeeka. Nilishuhudia vita, Nilionja amani. Sitawahi kusahau familia zilizofiwa, wazazi na watoto waliolipia gharama kubwa kwa vita hivyo. Na maisha yangu yote sitakoma kuitisha amani, kwa niaba ya vizazi vijavyo. Naomba sisi sote tuuungani mikono na kufurahi kwa sababu ni wajibu wetu kufanya hivyo kwa niaba ya watoto wetu.
Na kwa upande wake Bwana Abbas aliombea amani katika mkutano huo," alisema Peres.

Naye kiongozi wa Palestina, Mahmoud Abbas, aliomba kwenye hafula hiyo.

"Ee Bwana, tuletee amani ya kudumu na ya haki katika taifa letu na eneo letu, kwa ujumla, ili watu wetu na watu wote wa Mashariki ya Kati na Dunia nzima ifurahie matunda ya amani, utangamano na kuishi kwa pamoja kwa upendo.
Baada ya sherehe hiyo, iliyoshirikisha maombi ya Kikristo, Kiyahudi na Kiislamu, waliokuwepo walisalimiana kwa mikono na kupanda Mzaituni katika Medani ya Vatican kama ishara ya amani.
Papa ametangaza hadharani kuwa hataki kuingilia moja kwa moja mashauriano ya amani ya Mashariki ya kati, yaliyoporomoka Aprili lakini akasema kuwa anatarajia kwamba mkutano katika Vatican utapunguza uahasama kati ya pande hizo mbili kinzani za Mashariki ya Kati.

Friday, 6 June 2014

walioshiriki mbio za mita mia nne bonanza la ajtc hawa hapa

baadhi ya wanafunzi walioshiriki mbio za mita mia nne

kwa upande  wa wanawake ambao wameshiriki  wasichana nane na kuibuka msichana mmoja  kuibuka kidedea ambaye ni  editha mshana  na wasichana wengine kuishia njian.

 Hata hivyo  pia kwa upande  wa wavulana nao alipatikana mshindi ambaye aliwaacha kwa umbali mrefu ambapo alipatikana mshindi ambaye ni Ayubu martin aliyeibuka kidedea hapo jana.

mtawa anyakuwa ushindi wa uimbaji italia




Mtawa wa Italia anyakua ushindi


Mtawa mmoja kutoka Italia ambaye alipata umaarufu katika mtandao wa kijamii ameshinda shindano la kuimba nchini humo.
Mtawa huyo, Sister Christina Scuccia alitokea kwa mara ya kwanza katika

Ni uhalifu kuwanyanyasa wanawake - Misri


 


wanawake wa misri

Kwa mara ya kwanza Misri imepitisha sheria inayotaja unyanyasaji wa wanawake kuwa uhalifu.
Chini ya sheria hiyo wanaume watafungwa miaka 5 gerezani kwa kuwanyanyasa wanawake hadharani au faraghani.
Sheria hiyo imepitishwa kama hatua ya mwisho kuchukuliwa na rais anayeondoka wa Misri Adly Mansour.
'Unyanyasaji umezidi'
Watetesi wa haki za wanawake nchini Misri wamesema kuwa unyanyasaji wa wanawake umefikia viwango vya kuhuzunisha. Utafiti uliofanywa umeonesha kuwa karibu wanawake wote wa Misri wamewahi kupitia unyanyasaji wa aina fulani iwe ya matusi au hata ubakaji.
Utafiti huo umeonesha kuwa hata mavazi ya kufunika mwili wote yanayopendekezwa na sheria za kiislamu nchini humo, hazijawazuia wanaume hao kuwanyanyasa wanawake.
Na sasa inahofiwa kuwa mapinduzi waliofanya mwaka wa 2011 hayakuleta mabadiliko yoyote.
Wanawake wengi wamelalamika kuwa walinyanyaswa wakiwa katika maandamano katika midani ya Tahrir.
'Tatizo liko kwa itikadi mbovu'
Watetesi hao wa haki wanasema kuwa polisi mara nyingi wanawalaumu waathiriwa kuliko wale wanaofanya uhalifu huo.
Sasa sheria hii inachukuliwa kama hatua kubwa sana kusaidia tatizo hilo, ila hofu ni kwa utekelezaji wake. Wadadisi wanasema kuwa itakuwa vigumu zaidi kubadilisha itikadi za watu juu ya unyanuasaji wa wanawake nchini hum.