Ugali wa muhogo unaliwa sana na makabila mengi lakini tumeona kabila la waha kutoka Kigoma ndiyo asili yao.moja kwa moja tukaanze kuandaa mchemsho wa kuku.
MAHITAJI
Kuku wa kienyeji
Limao
Vitunguu
Pilipili
Tangawizi
Chumvi
Kisamvu kilichochemshwa
Karanga iliyosagwa
Nazi
Unga wa muhogo
Moja kwa moja tunaanza kumchemsha kuku wetu nitamuandaa kwa kumkata kata vipande kisha namuweka katika sufuria.kama tujuavyo kuku lazima akichemshwa lazima awekwe tangawizi ingawa kunasbaadhi ya watu hawapendi lakini ni vizuri ukaweka tangawizi kwa sababu ni kiungo ambacho kinasaidia sana kuleta hamu ya kula unaweza ukamla kuku mzima peke yako hahahahahahahahahahhah(natania).pia tangawizi utaweka ambayo tayari imetwangwa na siyo ya kusaga baada ya hapo unaweka maji na chumvi kiasi
Kuku wa kienyeji ni mgumu sana hivyo lazima uhakikishe kaiva vizuri hatua ya mwisho unamuweka limao na pilipili alafu unafunukuka kwa dakika 15 kumbuka uwingi wa pilipili unatokana ulaji wako pia unaweza kuweka viazi a ndizi baada ya hapo ipua mboga yako itakuwa tayari unaweza ukainywa kama supu. Kwa wale wenye waume wanaokunywa pombe unaweza ukamwandalia akanywa badala ya kwenda baa akanywa kwa raha zake.
Baada ya hapo ntaenda kukuandalia kisamvu, nitaanza kwa kukichemsha kisamvu changu kwa saa nzima baada ya hapo ipua kitakuwa tayari kwa kuunga anza kwa kubandika sufurua jikoni kisha weka vitunguu vikibadilika rangi na kuwa kahawia weka kisamvu chako na uache vichemke kwa sekunde kadhaa, baada ya hapo weka tui la nazi ambapo unatakiwa ukoroge taratibu ililishikane vizuri na mboga alafu unamalizia kwa kuwaka karanga baada ya hapo utaacha vichemke mpaka ile harufu ya ubichi itoke kabisa. Kisamvu chako kitakuwa tayari kupakuliwa na kuwekwa mezani.
Tunamalizia kwa kuandaa ugali wa muogo jamani wasomaji wangu kama tujuavyo ugali wa muhogo unapikwa tofauti na ugali wa kawaida, ugali huu unaanza kwa kubandika sufuria jikoni na kuweka maji kiasi baada ya kuchemka maji hayo utaweka unga kiasi ambao utasongea ugali wako lakini usikoroge funika kwa dakika chache kisha uanze kusonga utaona kama unavutika yani hauna desturi ya kuachana kama ugali wa sembe hivyo usiache kusonga mpaka utakapo hakikisha kuwa unga wote umegusa maji kumaanisha hauna mabuja utatumia kama dakika kumi kuwa tayari.Chakula hiki kinalika na rika lolote kumaanisha mtoto hata mtumzima.
No comments:
Post a Comment