
Serikali ya Rais Museveni inategemea kipato chake zaidi kutoka mkusanyo wa kodi
Bajeti katika
nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zinatarajiwa kutangazwa. Ni wakati
ambapo mizani ya matumizi na mapato ya serikali huanikwa hadharani.
Biashara katika Jumuiya imekuwa mhimili imara wa uchumi wa nchi ya Uganda kukua, licha ya msukosuko katika masoko ya dunia.Hali ni hiyo hiyo nchini Uganda kwa mujibu wa mwandishi wetu wa Kampala Ali Mutasa.
Kiokozi cha Uganda kiuchumi, kwa mujibu wa Rais Yoweri Museveni - ni Kilimo, Viwanda, Huduma, na Tetama - yaani, teknolojia ya taarifa na mawasiliano (ICT).
Katika sekta hizo zote nne, mali huzalishwa na nafasi za kazi hubuniwa. Hivyo bajeti ya mwaka 2014/15 itamakanikia sekta hizo nne.
Mwaka huu wa fedha, ingawaje, wafadhili waliikatia misaada bajeti - karibu robo.

Uganda ilipitisha sheria kali zaidi dhidi ya wapenzi wa jinsia moja
Labda bajeti itaongelea kirefu athari ya kukatwa msaada huo.
'Faida ndogo, kipato kidogo'
Kipato cha serikali zaidi kinatokana na kodi. Zaidi ya thuluthi mbili mwaka huu wa fedha serikali ikitegemea mkusanyo wa kodi, zaidi ya trilioni 8.
Lakini kukazuka tobo la kama $milioni 148, sababu ya baadhi ya makampuni kushindwa kulipa kodi.
Mojawapo ya sababu ni vita vya Sudan Kusini ambavyo vilivuruga biashara na Uganda, iliokuwa karibu $1bn, kila mwezi.
Uchumi haukukua kwa karibu 7%, badala yake ulizidi 5%, hii ikimaanisha faida za makampuni fulani zilikuwa chini hivyo kipato cha serikali kupungua.

Shilingi ya Uganda imeshuka dhidi ya sarafu kama dola ya Marekani
'Kupanda kwa gharama ya maisha'
Thamani ya shilingi iko chini kulingana na fedha ngumu kama dola, na hivyo kuyafanya maagizo kuwa ghali zaidi, mfano petrol au magari ambayo huagizwa kutoka nje.
Matokeo yake ni nauli kuwa juu na bei za vitu kupanda, japo serikali inasema inadhiiti vyema mfumko wa bei ambao uko kasoro ya 6%.
Ingawaje serikali ya Uganda, inatazamia mafuta kuanza kuuzwa mwaka huu wa fedha, huenda ikaamua kugharamia matumizi yake muhimu si kwa kupandisha zaidi kodi, bali kwa kupata mikopo katika masoko ya fedha ndani na nje ya Uganda.
Kwa mfano, mikopo inachangia kasoro ya 30% ya zao ghafi la ndani Uganda - ni kiwango cha chini, kulinganisha na Kenya 50% na Tanzania 40% hivi.
Ingawaje, mfuko wa fedha wa kimataifa, IMF na Benki ya Dunia na wadeni wengine wataiwasa Uganda isiandame mkondo huo wa madeni.
No comments:
Post a Comment