Thursday, 5 June 2014

Bashar Al Assad ashinda uchaguzi Syria

Assad ashinda Uchaguzi
Maafisa nchini Syria wamesema kuwa Bashar Al Assad amechaguliwa tena kama rais wa nchi hiyo.
Assad amepata asili mia 89 ya kura zote. Uchaguzi huo umefanyika katika mazingira ya vita vya wenyewe kwa wenyewe na inaaminika kuwa wraia waliokuwa katika maeneo yanayoshikiliwa na serikali pekee ndio waliofanikiwa kupiga kura.
Upande wa upinzani ulisusia uchaguzi huo wakiutaja kuwa kejeli kwa demokrasia. Upande wa serikali hata hivyo umesema kuwa uchaguzi huo umepata kuungwa mkono na wengi zaidi waki kisia kuwa asili mia 73 ya raia walijitokeza kupiga kura.
Tnagu kutolewa matokeo hayo, wafuasi wa rais Assad wamekuwa wakisherehekea katika barabara za Damascus.
CHANZO BBC

No comments:

Post a Comment