
Blatter adokeza nia yake kutaka urais wa Fifa kwa muhula wa 5.
Rais wa shirikisho la kanda FIFA, Sepp Blatter, amesema yuko tayari kuendelea na wadhfa huo kwa muhula mwengine wa 5.
Akizungumza katika kikao maalum cha Fifa huko
Sao Paulo amesema yuko tayari kugombea tena cheo hicho kama rais wa
shirikisho hilo kubwa linalosimamia soka ya dunia.
Europa imemtaka Blatter ajiuzulu kufuatia tuhuma za rushwa katika Fifa.
Blatter pia amependekeza kuwa mameneja wa timu waruhusiwe kutafuta haki pale kwa kutumia technologia pale watakapohisi maamuzi ya refa hayakuwa sawa.
Tisho la Maandamano
Wakati huo huo watu 10 wameripotiwa kukamatwa na kupelekwa vituo vya polisi huko Rio de Janeiro ili kuhojiwa kuhusiana na kushiriki kwao katika maandamano yenye ghasia.
Ulinzi unaendelea kuimarishwa hasa katika miji ya Sao Paulo na Rio ambako baadhi ya makundi ya watu wametishia kufanya maandamano kudai maslahi yao, wakati wa ufunguzi wa kombe la dunia utakaofanyika chini ya saa 24.
No comments:
Post a Comment