huwa hapendi kupitisha huu mda na kama akipitisha basi ita kuwa ni kwa bahati mbaya.
Leo twende tukaone pishi la dagaa waliopikiwa mafuta ya mawese. pamoja na ugali wa dona naamin utafurahi sana kuona chakula hiki na endapo ukipika nyumbani mwako utakifurahia saaanaaaaaaaaaaaa
MAHITAJI
dagaa
nyanya
vitunguu
hoho
karoti
mafuta ya mawese
chumvi
unga wadona
JINSI YA KUANDAA
unachambua dagaa wako vizuri unatoa vichwa na wengine huwa hawatoi vichwa lakini tunafanya hivi ili kupunguza michanga nadagaa pia waweza kupika wa wa mwanza wale wadogo au wakubwa wa kigoma
unaziweka kwenye kikaango kwa ajili ya kuwababua kidogo baada ya hapo unaziweka katika maji ya uvuguvugu lengo ni kuziosha na kama kuna michanga imebaki kwenye dagaa huwa inatoka kwa urahisi wakati wa kuziosha baada ya hapo unaziweka kwenye bakuli safi
unaweka kiasi cha mafuta kwenye sufuria ya kupikia unatenga jikoni kwenye moto yaanze kuchemka hadi uone povu ila hakikisha hayabadiliki rangi yake ya kawaida ya njano baada ya hapo unakatia kitunguu pamoja na karoti pamoja na dagaa unaanza kukoroga taratibu mpaka uone dagaa wanaanza kukauka baada ya hapo unaweka nyanya kwenye huo mchanganyiko wako unasubili kwa dakika chache kisha mboga yako itakuwa tayari kwa kuliwa na ugali wako wa dona
Siyo mbaya ukanywa na juisi yako baada ya kula chakula chako hicho
No comments:
Post a Comment