.jpg)
Mtendaji Mkuu wa Tanroads, Patrick Mfugale
Ili kupunguza foleni jijini Dar es Salaam Wakala wa Barabara nchini (Tanroads), umetangaza kujenga barabara sita katika jiji.
Mikataba ya ujenzi huo ilisainiwa jana jijini na kampuni mbili zimepewa kazi ya kujenga barabara hizo kwa kiwango cha lami.
Mtendaji Mkuu wa Tanroads, Patrick Mfugale alitaja barabara zitakazojengwa kuwa ni Goba hadi Mbezi Mwisho yenye urefu wa kilomita saba, Tangibovu Samaki Wabichi hadi Goba yenye urefu wa kilomita tisa.
Kampuni zilizopewa kazi hiyo ambayo inaanza baada ya kusainiwa mkataba ni Estim Constuction Co. Ltd na Hari Singh & Sons Ltd.
Alitaja barabara nyingine kuwa ni pamoja na Kimara Baruti hadi Msewe yenye urefu wa kilomita 2.6, Kilungule hadi External hadi Maji Chumvi yenye kilomita tatu, Kifuru Kinyerezi kilomita nne na Tabata Dampo hadi Kigogo yenye kilomita 1.6
Alisema ujenzi huo utakamilika baada ya mwaka mmoja kuanzia sasa na kwamba zitasaidi kutatua tatizo la usafiri katika maeneo hayo.
Aidha, Mfugale alisema serikali inatarajia kujenga barabara mpya ya kutoka Chalinze hadi jiji Dar es Salaam ambayo itakuwa ya kulipia kwa kila gari litakaloitumia.
No comments:
Post a Comment