Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu
Joseph Warioba, akimsikiliza Profesa Issa Shivji baada ya ufunguzi wa
kigoda cha sita cha Mwalimu Nyerere uliofanyika jana kwenye |
Profesa wa mwaka wa Kigoda cha Mwalimu Julius Nyerere, Profesa Patrick Loch Otieno Lumumba (PLO), ameshangazwa na kile kinachoendelea barani Afrika kwa Waafrika wenyewe kutojiamini na hivyo kuenzi utumwa kwa kuamini mambo ya mataifa ya Magharibi kuwa ni bora zaidi kuliko yale wanayozalisha wao wenyewe.
Kwa mujibu wa Profesa Lumumba, kwa kufanya hivyo, Waafrika hawaenzi jitihada zilizoanzishwa na waasisi na wapigania uhuru wa mataifa ya Afrika wakiwamo hayati Julius Nyerere (Tanzania) na Kwame Nkuruma (Ghana) ambao walisisitiza ukombozi wa Afrika kifikra, kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Profesa Patrick Lumumba, ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shule ya Sheria nchini Kenya, alibainisha hayo kwenye Tamasha la Sita la Kitaaluma la Kigoda cha Mwalimu Nyerere katika Taaluma za Ujumuishi wa Afrika, lililofanyika jana Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Alisema Waafrika wanazo hospitali na madaktari wazuri lakini wanapoumwa wanakwenda kutibiwa nje kwenye hospitali za mataifa ambayo walikuwa wakoloni wao.
Alisema, haiwezekani kwa nchi za Afrika kuwa na vyuo vyao vikuu ambavyo vinazalisha wataalamu wazuri wakiwamo wahandisi lakini wanaotengeneza barabara zao ni Wachina, Wajapani na Wakorea na kuwaacha wale waliowazalisha wenyewe.
Alisema Waafrika wako radhi kushabikia michezo, wachezaji, sherehe za watu maarufu na tamaduni za mataifa mengine kuliko ya kwao kwa sababu ya kutojiamini na kukosa uzalendo kwa nchi zao.
“Afrika ina vyuo vikuu vingi, mainjinia wengi, lakini wanaotengeneza barabara wanatoka nchi zingine. Afrika inazo hospitali kubwa kama Muhimbili, Kenyatta lakini Waafrika hao hao wanapoumwa wanakwenda kutibiwa nchi za nje zilizokuwa wakoloni wa nchi zao,” alifafanua Lumumba na kuongeza:
“Mifumo ya elimu imebadilishwa na kusisitiza lugha za kigeni kikiwamo Kiingereza kuwa ndiyo muhimu kuliko za kiafrika. Mwalimu Nyerere alisisitiza sana kuhusu elimu kwa ajili ya kuleta mapinduzi ya fikra ndiyo maana alianzisha Azimio la Arusha.
No comments:
Post a Comment