Thursday, 5 June 2014

fahamu Jinsi ya kuondoa harufu mbaya kwenye kwapa

Jinsi ya kuondoa harufu mbaya kwenye kwapa

Kwapa ni moja ya maeneo yanayoweza kuleta karaha kutokana na baadhi ya watu kukabiliwa na harufu mbaya.
Zipo sababu mbalimbali zinazochochea tatizo hili, moja kubwa kati ya hizo ni uvivu wa kuoga na kuacha nywele nyingi kwapani. Wakati mwingine huachwa hivyo hadi kubadilika rangi na kuwa nyeupe au njano na kujisokota.
Mtu anapotoa jasho, bakteria wanatumia nafasi hiyo kwenda kwenye jasho kujipatia chakula. Kadiri vijidudu hivyo vinavyozidi kuwa vingi harufu nayo inazidi.
Kwa kawaida, jasho lina kawaida ya kukaa kwapani zaidi kuliko sehemu yoyote mwilini na kuwepo kwake eneo hilo kwa muda mrefu, husabisha harufu kali inayoweza kusababisha mtu kukosa raha.
Baadhi ya watu wamekuwa wakikabiliana na tatizo hilo kwa kutumia manukato na maji ya marashi kuondoa tatizo hilo.
Hata hivyo, kutumia manukato na maji ya marashi pekee, haviwezi kuwa njia pekee yenye kuaminika katika kutafuta tiba na suluhu ya tatizo hilo linalosababishwa na uchafu.
Moja ya njia za kukabiliana na tatizo hilo ni kuoga maji mengi kwa kutumia sabuni iliyotengenezwa kwa kutumia magadi. Kwa kiasi kikubwa, magadi yana uwezo wa kupambana na bakteria ambao hujificha kwenye kwapa na kusababisha kutokea kwa harufu kali.
Pili ni muhimu kuhakikisha kwapa linakuwa safi wakati wote, ikiwezekana kunyoa kila baada ya wiki moja na baada ya kunyoa unaweza kupaka mafuta ya nazi ili kuondoa muwasho.
Njia nyingine ni unywaji wa maji mengi, kwani kwa kiasi fulani yanasaidia kutoa sumu kwenye mwili na kusababisha harufu kupungua.
Pia unaweza kutumia limao au ndimu kukata harufu ya kwapa. Kata limao au ndimu nusu kwa kisu kisha paka kipande cha limao ulichokata kwenye kwapa lako na hakikisha unalisugua mpaka litoe maji yake. Weka kwapa lako lipate hewa ili hiyo juice ya limao uliyopaka ikauke.
Asidi citric katika maji ya limao inasaidia kutoa tezi ya jasho hivyo kuondoa harufu.
Angalizo: Kama unatumia kitaulo kujifuta maeneo ya kwapa hakikisha unakifua na kukianika kwenye jua ili kuua vijidudu vinavyojificha kwenye nguo hiyo

No comments:

Post a Comment