Monday, 14 July 2014

Kiwanda cha 'Samsung' chatumikisha watoto





Kampuni ya bidhaa za elektroniki ya, Samsung imesema kuwa imepata ushahidi wa kuwatumikisha watoto kinyume na sheria katika moja ya kiwanda cha kusambaza bidhaa zake nchini China cha Dongguan Shinyang .
Samsung imesema kuwa iliichunguza kampuni hiyo baada ya madai kutoka kwa shirika la kupambana dhidi ya utumkishaji wa watoto ya Marekani 'China Labor Watch' kuituhumu kwa kuwatumikisha watoto.
Awali kampuni hiyo ya korea kusini ilikana kwamba baadhi ya kampuni zinazosambaza bidhaa zake zinawaajiri wafanyakazi walio chini ya umri wa miaka 16,lakini uchunguzi uliofanywa na shirika hilo umeilazimu kampuni hiyo kukiri makosa yake.

Takriban watoto watano walio chini ya umri wa miaka 16 walikuwa wakitengeneza baadhi ya sehemu za simu za samsung ,kulingana na uchunguzi wa siri wa shirika hilo la haki za wafanyikazi,lililo na makao yake mjini New York.
Watoto hao ambao wamekuwa wakifanya kazi bila kandarasi wamekuwa wakilipwa thuluthi mbili za mshahara wa mtu mzima.

Wasambazaji wa bidhaa za Samsung wanashtumiwa kwa kuvunja sheria za kazi za uchina kupitia kuwaruhusu watoto wadogo kufanyakazi katika kemikali mbali na kupuuza sheria za uchina kuhusu kazi za mda wa ziada ambapo hufanya kazi kwa masaa 11 katika zamu ya masaa 10.

Hivi majuzi kampuni ya samsung ilitoa matokeo ya ukaguzi wake kuhusu wasambazaji wa bidhaa zake nchini Uchina ambayo hayakupata ushahidi wowote kuhusu ajira ya watoto.
kampuni hiyo imeahidi kukata uhusiano wake na kampuni za usambazaji wa bidhaa zake iwapo itathibitisha madai hayo mapya

Shinikizo wasichana kuachiliwa Nigeria





Malala na mmoja wa wazazi wa wasichana waliotekwa nyara Nigeria

Mwanaharakati mwenye umri mdogo raia wa pakistan Malala Yousafzai anatarajiwa kukutana na rais wa Nigeria Goodlack Jonathan mjini Abuja hiii leo kushinikiza kuchukuliwa hatua zaidi ili kuwakoa wasichana wa shule waliotekwa na kundi la wanmgambo wa Boko Haram mwezi April.

Tayari mwanaharakati huyo ashakutana na familia za wasichana hao kuonyesha uzalendo wake kwao.
Boko Haram wametoa kanda ya video ya kusuta kampeni za kutaka kuachiliwa wasiha hao mabpo kundi limetaka kuachiliwa kwa wapiganaji wake.

Malala alipigwa risasi kichani na kundi la Taliban nchini Afghanistan alipokuwa akipigania elimu kwa wasichana

Monday, 23 June 2014

Wandishi wa Al Jazeera miaka 7 jela


Mahakama nchini Misri imewahukumu jela miaka saba wandishi watatu wa habari wa shirika la habari la Al Jazeera waliokuwa wamezuiliwa kwa miezi sita nchini humo.

Walipatikana na hatia ya kueneza habari za kupotosha na kushirikiana na kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Muslim Brotherhood.

Mmoja wa wandishi hao ni Peter Greste, raia wa Australia na ambaye pia alikuwa mwandihi wa habari wa BBC wakati moja.

Thursday, 12 June 2014

Blatter Ataka muhula wa tano urais Fifa



Blatter adokeza nia yake kutaka urais wa Fifa kwa muhula wa 5.
Rais wa shirikisho la kanda FIFA, Sepp Blatter, amesema yuko tayari kuendelea na wadhfa huo kwa muhula mwengine wa 5.
Akizungumza katika kikao maalum cha Fifa huko Sao Paulo amesema yuko tayari kugombea tena cheo hicho kama rais wa shirikisho hilo kubwa linalosimamia soka ya dunia.
Kwa kutangaza hivyo ni kwamba amepuuzilia mbali kauli za maafisa wa soka wa Europa wanaomtaka ajiuzulu kufuatia madai ya rushwa yanayoiandama Fifa,wakati ilipochaguliwa Qatar kuwa mwenyeji wa kombe la dunia 2022.
Europa imemtaka Blatter ajiuzulu kufuatia tuhuma za rushwa katika Fifa.
Awali Blatter mwenye umri wa miaka 78 alikuwa amedokeza kuwa angestaafu baada ya kipindi chake cha sasa.
Blatter pia amependekeza kuwa mameneja wa timu waruhusiwe kutafuta haki pale kwa kutumia technologia pale watakapohisi maamuzi ya refa hayakuwa sawa.
Tisho la Maandamano
Wakati huo huo watu 10 wameripotiwa kukamatwa na kupelekwa vituo vya polisi huko Rio de Janeiro ili kuhojiwa kuhusiana na kushiriki kwao katika maandamano yenye ghasia.
Ulinzi unaendelea kuimarishwa hasa katika miji ya Sao Paulo na Rio ambako baadhi ya makundi ya watu wametishia kufanya maandamano kudai maslahi yao, wakati wa ufunguzi wa kombe la dunia utakaofanyika chini ya saa 24.

Ulaya wataka Blatter ajiuzulu kwa usemi



Rais wa Shirikisho la kandanda duniani, FIFA, Sepp Blatter.
Maafisa wa kandanda wa Europa sasa wamemtaka rais wa shirikisho la kimataifa la kandanda FIFA, Sepp Blatter, ajuzulu kutokana na madai ya rushwa yanayoindama Fifa.
Wametilia shaka uongozi wake.
Mkuu wa chama cha soka cha uholanzi Michael Van Praag, amesema chini ya uongozi wa Blatter ,Fifa imeandamwa na tuhuma za rushwa na ili Fifa kujisafisha ni sharti Blatter angatuke.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha soka Uingereza , Greg Dyke,amesthtumu kauli ya Blatter kuwa madai ya rushwa kuhusiana na kuchaguliwa kwa Qatar kuwa mwenyeji wa kombe la dunia 2022 yanayoripotiwa katika magazeti ya Uingereza yamechochewa na ubaguzi wa rangi.
Blatter anatarajiwa kutangaza nia yake ya kuwania nafasi kipindi cha tano kuingoza Fifa katika uchaguzi wa Fifa unaotarajiwa kufanyika mwaka ujao.
Kwa sasa wajumbe wa Fifa wanavikao huko Sao Paulo wakijiandaa kwa ufunguzi wa kombe la dunia hapo kesho ambako Sepp Blatter pia amekuwa akitoa cheche za maneno dhidi ya wale wanaoisema vibaya Fifa na Qatar.

Tisho la mgomo Uwanja wa ndege Rio


Makundi mbalimbali yamekuwa yakitumia ujio wa kombe la dunia kugoma kudai maslahi yao
Wafanyakazi wa kiwanja cha ndege cha Rio wametangaza mgomo wa saa 24 kuanzia usiku wa manane saa za Brazil.
Hii ni kumaanisha mgomo huo utaendelea hadi wakati wa ufunguzi wa kombe la dunia.
Japo sherehe na mechi ya ufunguzi zinafanyika mjini Sao Paulo, na ni asilimia 20% tu ya wafanyikazi ndio watakao goma, mgomo huo bila shaka utatatiza usafiri katika mji huo wa Rio ulio wapili kwa ukubwa nchini Brazil.
Wafanyikazi wanaoshughulikia abiria na mizigo na wale wanaofanya usafi wa hata ndegeni ni baadhi ya watakaogoma.
Afueni baada ya baadhi ya wabrazil wafanyikazi wa reli na mabasi kusitisha migomo ya kudai posho.
Sehemu za kuhudumia wageni wa kimataifa na wa ndani ya nchi zitatatizwa na mgomo huo.
Wafanyikazi hao wanadai nyongeza ya mshahara na posho za kufanya kazi wakati wa kombe la dunia wakisema kazi zimeongezeka.
Mmoja wa viongozi wa chama cha wafanyikazi hao , Luiz Braga, amekana wanatatiza kombe la dunia kwa maksudi, akieleza kuwa 'hatutaki kuharibu kombe la dunia, tunachofanya ni kudai haki zetu tu'.

Nchi za Afrika Mashariki kusoma bajeti

 
Serikali ya Rais Museveni inategemea kipato chake zaidi kutoka mkusanyo wa kodi
Bajeti katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zinatarajiwa kutangazwa. Ni wakati ambapo mizani ya matumizi na mapato ya serikali huanikwa hadharani.
Biashara katika Jumuiya imekuwa mhimili imara wa uchumi wa nchi ya Uganda kukua, licha ya msukosuko katika masoko ya dunia.
Nchini Kenya wananchi wanatarajia kuwa bajeti itaweza kuwalinda kutokana na mfumuko wa bei pamoja na kiwango kikubwa cha kodi inayotozwa.
Hali ni hiyo hiyo nchini Uganda kwa mujibu wa mwandishi wetu wa Kampala Ali Mutasa.
Kiokozi cha Uganda kiuchumi, kwa mujibu wa Rais Yoweri Museveni - ni Kilimo, Viwanda, Huduma, na Tetama - yaani, teknolojia ya taarifa na mawasiliano (ICT).
Katika sekta hizo zote nne, mali huzalishwa na nafasi za kazi hubuniwa. Hivyo bajeti ya mwaka 2014/15 itamakanikia sekta hizo nne.
Mwaka huu wa fedha, ingawaje, wafadhili waliikatia misaada bajeti - karibu robo.
Uganda ilipitisha sheria kali zaidi dhidi ya wapenzi wa jinsia moja
Si kwa sababu za kiuchumi, bali za kisheria; Uganda ilipoamua kupitisha sheria kali zaidi dhidi ya wapenzi wa jinsia moja.
Labda bajeti itaongelea kirefu athari ya kukatwa msaada huo.
'Faida ndogo, kipato kidogo'
Kipato cha serikali zaidi kinatokana na kodi. Zaidi ya thuluthi mbili mwaka huu wa fedha serikali ikitegemea mkusanyo wa kodi, zaidi ya trilioni 8.
Lakini kukazuka tobo la kama $milioni 148, sababu ya baadhi ya makampuni kushindwa kulipa kodi.
Mojawapo ya sababu ni vita vya Sudan Kusini ambavyo vilivuruga biashara na Uganda, iliokuwa karibu $1bn, kila mwezi.
Uchumi haukukua kwa karibu 7%, badala yake ulizidi 5%, hii ikimaanisha faida za makampuni fulani zilikuwa chini hivyo kipato cha serikali kupungua.
Shilingi ya Uganda imeshuka dhidi ya sarafu kama dola ya Marekani
Sekta binafsi ambayo inatiliwa shime na serikali pia inatapatapa kutokana na gharama kubwa ya mikopo, kwani kima cha riba ya benki kuu kikoo juu sana, 11%, na kuifanya mikopo katika benki za kibiashara kuwa ghali mno kwa wafanyabiashara wengi wadogowadogo, ambao ni mhimili wa uchumi.
'Kupanda kwa gharama ya maisha'
Thamani ya shilingi iko chini kulingana na fedha ngumu kama dola, na hivyo kuyafanya maagizo kuwa ghali zaidi, mfano petrol au magari ambayo huagizwa kutoka nje.
Matokeo yake ni nauli kuwa juu na bei za vitu kupanda, japo serikali inasema inadhiiti vyema mfumko wa bei ambao uko kasoro ya 6%.
Ingawaje serikali ya Uganda, inatazamia mafuta kuanza kuuzwa mwaka huu wa fedha, huenda ikaamua kugharamia matumizi yake muhimu si kwa kupandisha zaidi kodi, bali kwa kupata mikopo katika masoko ya fedha ndani na nje ya Uganda.
Kwa mfano, mikopo inachangia kasoro ya 30% ya zao ghafi la ndani Uganda - ni kiwango cha chini, kulinganisha na Kenya 50% na Tanzania 40% hivi.
Ingawaje, mfuko wa fedha wa kimataifa, IMF na Benki ya Dunia na wadeni wengine wataiwasa Uganda isiandame mkondo huo wa madeni.